Nikikuuliza unapenda kipi kutoka kwa
mpenzi wako najua wengi watatoa majibu tofauti tofauti wapo watakao
sema, mcheshi, anamvuto napenda anavyo tabasamu na vitu vingine kama
hivyo, LAKINI leo kupitia katika Mtembezi Mahaba karibu uyatambue mambo matatu muhimu ili kumdatisha mwenza wako.
1.UZUNGUMZAJI WAKO
Unavyozungumza na mpenzi wako ni tofauti kabisa na unavyozungumza
na watu wengine. Ni hatari sana kutumia lugha ya ukali ama isiyo
ya kiungwana kwa mpenzi wako. Unatakiwa kufahamu kwamba, mpenzi wako
ni mtu muhimu sana katika maisha yako hivyo unatakiwa kuwa makini
pindi unapozungumza naye.
Kuonesha kwamba wapo wasiojua
mapenzi ni nini, unamkuta mtu anamuita mpenzi wake majina kama vile
mshamba na mengine mengine kama hayo, Mpenzi wako kweli umuite demu? Na
wale wengine kule mtaani utawaita nani?
Huo si ustaarabu na kamwe
mapenzi yenu hayawezi kushamiri kwa mtindo huo, Kuna wengine matusi haya
waishi midomoni mwao. Kwa kufanya hivyo jua tu kwamba una mboa laazizi
wako. Aidha mapozi katika uzungumzaji wako ni miongoni mwa vitu
vinavyoweza kumdatisha.
2.TABIA ZAKO
Huu ndio msingi imara wa
uhusiano wa kimapenzi. Wapo wanawake ambao ni wazuri na wenye kila sifa
ya kuwa na wapenzi bora, lakini kutokanana tabia zao chafu wamekuwa
wakiachwa kila wanapoingia katika uhusiano.
Nani atakupenda na kudiriki
kuendelea kuwa katika uhusiano na wewe kama tabia zako si nzuri? Wengi
wetu tunapenda kupata sifa ya kuwapata wapenzi ama wachumba wenye tabia
nzuri ili tuweze kusifiwa na marafiki zetu pamoja na wazazi.
Kwa maana hiyo basi, kuwa
makini sana na tabia ambazo unajua haziwezi kumvutia mpenzi wako ama
jamii inayowazunguka kama vile WIVU uliopitiliza kiasi cha kuwa kero,
kutaka makuu pamoja na tamaa zisizo na msingi.
Nimeweka wivu juu kutokana na
ukweli kwamba, kuna wanawake hata wakiwakuta wapenzi wamesimama ama
kupigiwa simu na mtu wa jinsia tofauti bila kujua ukweli wa mambo
wanaanzisha vurumai, huu ni ulimbukeni.
3.JINSI UNAVYOMRIDHISHA
Yote hayo hapo juu ni tisa,
lakini kumi ni jinsi unavyoweza kumridhisha mpenzi wako hasa mnapokuwa
faragha mkipeana raha za dunia.
Hata kama una tabia nzuri na
umbile la kumvutia kiasi gani, kama huna utaalam na ujuzi wa kutosha
katika kumpa raha mpenzi wako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa,
lazima penzi ama ndoa yako itakuwa na walakini.
Lakini kitu ambacho kimekuwa
kikiwavutia walio wengi waume kwa wanawake ni utundu na ubunifu wakati
mnapokuwa faragha. Kinachotakiwa ni kupeana kile roho inataka ili suala
la kusalitiana lisiwepo.
Comments
Post a Comment