SABABU 10 KWANINI UMUACHE MWANAUME ULIYENAYE

Kumbuka kuwa kuna mtu maalum kapangwa kwa ajili yako, muda utafika tu na utapata furaha unayoitafuta, usiogope kuanza upya kama ulipo hapakufai maana siku zote tambua mapenzi hayalazimishwi kwa namna yoyote ile. Zifuatazo ni sababu zinazokulazimu umuache uliyenae katika mahusiano.black-couple-5

1. Kila mara ukiwa nae ndani na mnafanya mapenzi au anakubusu, anajisahau na kukuita jina lisilo lako, huyo bado hajatulia na hajakuweka kwenye mipango yake bado, MUACHE, ukilazimisha sana utapotea.

2. Upo nae lakini kila mara unapowaza mipango yako ya baadae humuweki kwenye mipango yako na hata unapokuwa naye mawazo yako muda mwingi yanakuwa mbali, HUYO SI CHAGUO LAKO, muache uendelee na safari.black-couple-2

3. Kila unapokuwa naye, simu yake inakuwa yake na simu yako inakuwa yake pia, anasoma sms na kuwa mkali sana kwenye simu yako ilhali yako wake huruhusiwi hata kuigusa, hakufai huyo.

4. Kila unapokuwa na ugomvi nae kila siku wewe ndio wa kumuomba msamaha hata kama yeye ndio amekukosea, huyo hawezi kuwa na upendo wa kweli, mapenzi ni kusikilizana pande zote mbili na si kwa upande mmoja kuonewa kwa kila kitu.black-couple-4

5. Kuvaa ni njia mojawapo ya kujiamini kwa mwanamke, lakini inapotokea anakupangia kila vazi unalotakiwa kuvaa na usilotakiwa kuvaa hapo inakuwa sio sawa, huwezi kutoka kwenda shule, kazini, outing, na kwingineko mpaka aone ulichovaa.

6. Anakuchagulia watu wa kuwa nao ikiwa ni pamoja na marafiki, hii sio dalili nzuri, wanaume wanaotenda ‘madhambi’ pembeni ndo huwa na tabia hii kwa wingi, wewe unakuwa ni mtu wa kubadili marafiki kila kukicha.BLACK COUPLE

7. Linapokuja suala la pesa mara nyingi huwa hakuna undugu, mara nyingi amekuwa ni mtu wa kukukopa pesa lakini anajifanya kusahau inapokuja muda wa kulipa deni, sio dalili nzuri ya mwanaume anayekufaa, una mipango yako binafsi ukiachilia mbali mapenzi na yeyote atakayesababisha mipango yako kutosogea mbele hatakiwi kuvumiliwa.

8. Mapenzi yake kwako huongezeka pale tu anapokuhitaji kwa ajili ya kutimiza haja zake za ngono na anapomaliza hukusahau na kukupotezea, hakufai kabisa huyo mtu.black-couple

9. Kila unachomwambia hukusikiliza na kukubaliana nawe lakini inapokuja wakati wa kutekeleza kwa vitendo mlichokubaliana mambo huwa tofauti, ANAKUDHARAU na anajisemea moyoni Bora Liende, hakufai huyo.

10. Hawezi kila kitu cha jikoni, hawezi kuosha vyombo hata kikombe cha chai, hawezi kupika hata chai, hawezi hata kufua nguo zake za ndani na anaona kama kazi hizo zote ni za wanawake tu, umejaribu sana kumuelekeza na haonyeshi mabadiliko, Kimbia.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016