Mwanamuziki Billnass Awa Lulu , Label Kubwa za Mziki Zamgombania Bongo
Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label yake ya ‘LFLG’, ameiambia Bongo5 kuwa kuna label nyingi zinamtaka kufanya naye kazi.
“Kusema kweli kuna mambo makubwa yanakuja, huwenda kazi yangu mpya ikaja nikiwa ndani ya label mpya,” alisema Billnas. Kuna label nyingi zimekuja na bado nipo kwenye mazungumzo, nadhani muda ukifika mtasikia tu,”
Billnas alianza kufanya vizuri na wimbo ‘Ligi Ndogo’ akiwa Rada Entertainment lakini baadae alihama katika label hiyo na kuanzisha label ya ‘LFLG
Comments
Post a Comment