Kama Wewe Mwanaume Una Tatizo la Kufika Kileleni Haraka Kabla Mpenzi Wako Hajaridhika Hii Inakuhusu
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.
Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.
Kimsingi mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}
Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.
Kupiga punyeto au kujichua;
mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabiaile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.
Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa;
kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.
Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa;
mtu akiwa na historia ya kupata hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.
Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu;
baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.
Kurithi;
baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.
Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.
Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.
Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.
Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.
Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.
Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.
Punguza wasiwasi:
hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu, hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.
Fanya taratibu:
picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.
Badilisha style:
ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.
Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa
Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.
Fanya na kuacha:
hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.
Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.
Tumia kilevi:
unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.
·
Matibabu ya kutumia dawa.
hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...
1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.
2. anesthetic creams: hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.
Comments
Post a Comment