Yapo mambo mengi yanayotokea kila siku katika maisha ya mapenzi,
mambo hayo yana wezekana kuwa ni ya lazima kutokea, unayasababisha
mwenyewe au unaruhusu yatokee bila ya sababu.
Kutokana na hayo yote, leo
nitazungumzia baadhi ya wapenzi wenye tabia za kutoa mambo yao ya
faragha na kuyapeleka kwa mashoga au rafiki zao.
Kila unachokifanya usiku, mchana au
asubuhi na mpenzi wako, basi mama au baba wa jirani anafahamu,
mkikwaruzana kidogo, ukimnyima mwenzio haki yake ya ndoa, basi mama au
baba mwenye nyumba anajua kila kitu kilichotokea.
Sidhani kama ni sawa, hili ni tatizo ni
moja ya upungufu mkubwa katika uhusiano, sasa utofauti wenu mkiwa
mmevaa na mkiwa watupu uko wapi ikiwa kila kitu unaenda kukianika kwa
rafiki zako?
Unadhani yeye hapendi vitamu na vizuri
au raha kama ambazo umekuwa ukimsimulia? Unadhani yeye hapendi raha na
ujuzi ndani ya sita kwa sita!
Usitengeneza mazingira ya kumshawishi
mtu dhidi ya mpenzi wako, ya chumbani yabaki kuwa ya chumbani na ya
sebuleni yawe ya sebuleni, pia ya kijiweni au saluni yaishie huko huko.
Usichanganye ya chumbani na sebuleni au saluni kuwa sehemu moja, utakuwa
umeharibu sana.
Kama kuna kosa kubwa ambalo ulikuwa
hulijui linaweza kukumaliza kwenye uhusiano basi ni mwanaume au mwanamke
kuwasimulia rafiki zake kuwa mumewe au mkewe anayaweza mambo fulani au
ana upungufu fulani.
Kwanza inashangaza sana unawezaje
kusimulia mambo nyeti kiasi hicho, mambo ya faragha ni siri kama ilivyo
usalama wa taifa, ndivyo ambavyo unapaswa kuiona kuwa ni sekta nyeti
sana.
Kwa kweli inasikitisha kuona kila unachofanyiwa na mpenzi wako unakwenda
kuwaambia mashoga zako. Eti, ooooh! Jana bwana’angu kanifanyia hivi,
kanigeuza hivi, kiukweli usiku wa jana nimeinjoy sana.
Kwa penzi la mpenzi wangu, nashukuru
Mungu nimempata mpenzi anayeyajua mambo, kwa hilo sina shaka
kabisa, Tabia hii ipo kwa pande zote mbili, wanaume kuhadithiana na
hata wanawake pia kufanya hivyo, lakini siyo wote. Unakuta kijana
yuko kijiweni na washikaji zake kakazana kuwasimulia wenzake, Mwajuma
ni mjuzi faragha, anajua kuzungusha nyonga hakuna mfano wake,
mwanangu yaani nashindwa namna ya kuelezea wewe elewa mambo anayaweza.
Comments
Post a Comment