Kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda
hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume
kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndio
umeshapenda.
Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia
katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume
unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ana mpenzi wake
yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika
maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Utapambana kuhakikisha unapata kile
ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi
kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta
upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa
na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.
Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu
ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye
‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo
uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future
naye.
Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba
uhusiano wao hauko ‘serious’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na
likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na
wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye
na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake?
Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu
anayeonesha kukumisi
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda
anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana
‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza
kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako.
Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye
tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
Comments
Post a Comment