MAMBO SITA KICHOCHEO CHA USALITI



Hakuna kitu kinachoumiza kwenye mapenzi kama wenza kusalitiana, kwa mtu anaingia kwenye mapenzi akiwa anaimani kuwa mpenzi wake anampenda kwa dhati, swali la kujiuliza ni mambo gani ni kichocheo cha usaliti, fuatana nami katika makala hii.black-couple-cheater

1. Kutokuvutia tena
Moja ya sababu iliyopelekea kukubali kuoa au kuolewa na huyo mwenzi wako, kuna baadhi ya vitu ulivutiwa navyo ndio akawaacha woote na kumchagua huyo.  Vitu hivyo usipovizingatia na kuvi “maintain” vitasababisha hali ya kukinai kwa mwenzi wako na mwisho kuanza kuvutiwa na wengine kule nje.

2. Kutokujali tena kuwa unaongezeka unene, kubadilika unavyoonekana.

Kila mwanandoa ana “test” yake ya mvuto kwa mwenzi wake, Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya wembamba wako sasa unapojiachia na kuwa mnene ila hamu ya kuendelea kuvutiwa nawe inapungua na baadaye inakwisha na kusababisha aanze kuchungulia nje.

• Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya unene au kujazia katika maeneo Fulani Fulani. Sasa mwili ukiporomoka unapoteza ule mvuto tena na kumfanya apoteze hamu ya kuwa na wewe na kumfanya kuanza kuchungulia chungulia nje.

• Ni vizuri kujali afya yako na kujua ni vitu gani vinavyomvutia mwenzi wako kutoka kwenye mwili wako na ujitahidi kuvitunza “maintain” ili kuendelea kudumisha ule mvuto kwa mwenzi wako.black-couple-arguing-pf1

3.  Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.
Tendo la ndoa ndio mhimili unaoishikilia ndoa. Ukiona hamu ya tendo la ndoa imepungua kwa mwenzi wako ujue majanga yanakunyemelea, Kufanya tendo la ndoa mara chache miongoni mwa wanandoa ni ufa wa kubomoa ukuta na ulinzi wa ndoa.

4. Kutokwenda na wakati haswa katika mavazi.

Hili hasa ni kwa wanawake, Kabla ya kuolewa ulikuwa unajitahidi sana kujilemba na kujitunza kila wakati ulikuwa safi na nadhifu. Mumeo kila akikuangalia mpaka haamini kama ni wewe aliyekuoa ukiwa mrembo na wa kuvutia, Unavaa nguo nzuri tu pale unapotoka kwenda kanisani au mtoko maalumu.

5.Kukosekana kwa mawasiliano, Mawasiliano yana husisha pande zote mbili kwa anayetoa na anayepokea, mathalani katika vitu vya kawaida kama kujuliana hali pindi mnapokuwa mbali hasa wakati wa kutimiza majukumu ya kila siku, mfano meseji ya kumuuliza mwenza wako ameshindaje na anaendelea vipi katika utekelezaji wa majukumu yake, hali ikibadilika humfanya mwenza kufikiria tofauti na kuona humjali hatimaye kuwa msaliti.

6. Kushindwa kuendeleza yale yanayompendeza kila mmoja wenu. Mnakubaliana mipango kama wanandoa lakini utakelezaji unakua mgumu, Mmoja anakuwa tayari kutekeleza na mwingine anashindwa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016