Tunapozungumzia mwanamke kukosa uwezo
wa tendo la kujamiiana hapa tunamaanisha anakuwa hana hamu ya tendo hilo
au hata akilifanya hafurahii.
Uwezo wa kufanya tendo la kujamiiana
kwa mwanamke tunategemea unapungua taratibu kuanzia umri wa miaka
hamsini, siyo unaisha ila unaanza kupungua taratibu kadiri umri
unavyosonga mbele hadi baadaye unaisha kabisa.
Katika umri huo ndipo tunategemea
kusikia mwanamke anaanza kusema hamu ya tendo hilo inapungua au
imepungua na hata akilifanya hafurahii kama zamani, hii inatokana na
upungufu wa vichocheo muhimu vya ‘Estrogen’ ambavyo ni lazima vipungue
katika umri huo ambao mwanamke tayari ameshafikia ukomo wa hedhi na
uzazi. Endapo vichocheo hivi vitaendelea kuwa juu katika umri huo au
ataviongeza, basi kuna hatari ya mwanamke kupata saratani ya mfuko wa
uzazi.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Hali ya kutohisi hamu ya tendo na
kutopata raha ya tendo ni ya kawaida katika umri mkubwa wa mwanamke
kuanzia miaka 50 lakini si ya kawaida katika umri wa chini ya hapo, siyo
kawaida kwa mwanamke wa umri wa miaka 20 hadi 48 kupata tatizo hili.
Endapo mwanamke wa umri huu atalalamika hali hiyo basi ni tatizo
linalohitaji uchunguzi wa kina.
Katika umri wa kuzaa, pale mwanamke
anapoendelea kupata siku zake kama kawaida tunategemea mwili wake upo
vizuri, homoni zake zinafanya kazi vizuri na anafurahia maisha yake.
Kutohisi hamu ya tendo la ndoa ni
kutopata hisia za kimapenzi hata akimuona mwenzi wake, akiguswa au hata
akiambiwa maneno ya mapenzi hapati hisia wala msisimko wowote wa
kimapenzi. Mwanamke asiyefurahia tendo la ndoa ni yule asiyefikia kilele
cha tendo hilo, mwanamke akifikia kilele hutoa majimaji na huwa na hali
ya kumaliza tendo na kupumzika lakini akiwa na tatizo hili hafikii
hapo na hufanya tendo hilo basi tu na humridhisha tu mpenzi wake.
DALILI ZA TATIZO
Mwanamke mwenye tatizo la kutohisi hamu
huwa yupo tu na anaweza kukaa muda mrefu hata zaidi ya mwaka bila
kufanya tendo hili na hana tatizo lolote, huendelea tu na shughuli zake.
Mwenyewe atakuambia labda mwenzake amuanze lakini vinginevyo hajisikii
hamu kabisa. Kitaalamu hawezi kupata tatizo lolote kiafya labda kama
yupo kwenye uhusiano ndiyo italeta mgogoro. Mwanamke asiyefurahia tendo
anaweza kuwa na historia ya kuwa na maumivu wakati wa tendo, kama
alishawahi kuingiliwa kwa nguvu au kama mwenzake yaani mume ana matatizo
wakati wa tendo aidha hawezi au hamfikishi mara kwa mara.
Kutofurahia tendo kwa muda mrefu
humuathiri mwanamke katika afya yake ya akili na hulifanya kwa
kujilazimisha. Wanawake wengi wenye tatizo hili chanzo huwa ni wanaume
kushindwa kumudu tendo hili.
MATIBABU NA USHAURI
Tatizo hili halina dawa maalumu, jambo
la msingi ni kujua chanzo chake na kukitibu. Uchunguzi utazingatia mambo
mbalimbali kutegemea na daktari atakavyoona inafaa.
Comments
Post a Comment