FAHAMU ATHARI ZA KITAMBI KIAFYA


Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi kikubwa.

Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani. Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.kitambi

Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.

Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango madhubuti kulikabili. Vitambi hupunguza maisha ya watu wenye hali hiyo ya afya, hivyo kusababisha upotevu wa rasilimali watu.

Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.

Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.kitambi

Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari na si mbogamboga na matunda.

Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu. Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.

MAGONJWA

Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya watu duniani kote. Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa ya moyo na kansa. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo na ndipo matatizo yanapoanza.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016