JE Mwanamuziki Billnass Amejiunga na Label ya The Industry ya Nahreel? Jibu Liko Hapa


Msanii na mtayarishaji wa muziki wa The industry, Nahreel ameweka wazi kuwa label ya The industry ina project nyingi na rapper Billnas anayefanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’.
billnas

Rapper Billnas hivi karibuni aliwapa taarifa mashabiki wake ujio wa project nyingi kutoka The industry.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nahreel amesema kwa sasa wana kazi nyingi na rapper huyo.

“Yeah Billnas na The Industry kuna kazi nyingi zinakuja, nisingependa kuziweka wazi kwa sasa kwa sababu ni mapema,” alisema Nahreel. “Lakini pia wasanii wa label ya The Industry tayari wana kolabo nyingi na wasanii wa kubwa hapa nchini, kwa hiyo naweza sema mambo mazuri yanakuja soon,”

Kwa upande wa Kundi la Navy Kenzo, Nahreel amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kazi mpya za kundi hilo.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016