Skip to main content
JE KUNA GHARAMA YA MKE KUMTII MUMEWE?
Siku zote katika Mapenzi bora usisaliti
kabisa maana kovu la usaliti huwa ni gumu kufutika katika akili ya
aliyesalitiwa, Ni vyema kila mmoja akawa na mtu sahihi, aridhike naye na
wajenge familia. Kovu la usaliti lina gharama kubwa kufutika.
Unaweza ukaomba radhi na mwenzako
akakuelewa lakini asirudishe imani kwako. Kila wakati atakuwa na
wasiwasi na wewe. Anajiuliza kama alikuwa anakuwa anakupa kila kitu na
ukamsaliti, kipi cha ziada atakachokufanyia na wewe usimsaliti? Maswali
kichwani mwake yatakuwa mengi kuliko majibu hivyo ili kuepusha hayo yote
yasitokee, bora usithubutu kabisa
kusaliti.
Kuna kasumba ambayo baadhi ya wanawake
wanayo. Utandawazi umewakolea kwelikweli. Wanataka kuona wanawapanda
vichwani wanaume zao. Eti mwanaume ammnyenyekee, amuogope, Amtii.
Anamjibu mwanaume kadiri anavyojisikia. Hataki kuona anazidiwa kitu na
mwanaume. Mwanaume akikasirika, akafoka kuhusu jambo fulani, naye
anafoka. Anaonesha kwamba hamuogopi, anaweza kumfanya lolote atakalo.
Kujishusha kwake ni mwiko. Anaendesha
mapambano na mumewe utafikiri akishinda kuna kombe anapewa. Anataka
kuhakikisha mumewe ‘anaufyata’ kwake. Anamjibu kwa nyodo mumewe mbele ya
majirani au marafiki zake bila hofu wala woga wa aina yoyote.
Suala la msingi ni kujiuliza, kwani
kuna gharama gani mke akimtii mumewe? Mke akipanda na mumewe anafikiria
nini? Hata kama ni ushindi, ukishamshinda mumeo, halafu nini kitafuata?
Wewe uwe mkubwa zaidi ya mumeo?Ukijishusha,
ukimheshimu mume mbona ina maana kubwa zaidi kuliko kutomtii. Itakuwa
na faidia ya kiasili lakini pia utakuwa umeenda sanjari na mpango wa
Mungu. Sisemi kwamba mwanaume hapaswi kumheshimu mkewe lakini mke
anapaswa kumheshimu zaidi mumewe.
Comments
Post a Comment