Mahsusi kwa watu wanaotarajia kuanzisha mahusiano thabiti na yenye
malengo pamoja na wale ambao tayari wamo ndani ya mahusiano ya aina
hiyo imekuandalia vitu vya kuzingatia karibu twende sawa.
KWA WATARAJIWA
1.Usidanganyike na muonekano wa nje au yale maongezi ya mwanzo, Kila mtu hua mstaarabu siku za mwanzo hata wale ambao sio.
2.Usikimbilie kutangaza nia haraka.
Siku zote ni rahisi mtu kua
muwazi kwa rafiki yake kuliko kwa mtu ambae anajua anataka mahusiano nae
kwa hofu ya kumpoteza.Tumieni muda wakutosha kufahamiana kama marafiki
kabla hamjajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi.
3.Uliza maswali kuhusu vitu ambavyo ni muhimu sana kwako.
Kwa mfano kama ni mtu wa familia au sio taka kujua mawazo yake
kuhusu watoto hii itaepusha migongano isiyo ya lazima hapo baadae.
4.Penda kujua malengo yake ya baadae.
Hii itakuwezesha kugundua ni mtu wa aina gani kama ni mpenda maendeleo,mtu wa starehe tu n.k.
5.Kuwa muwazi.
Hii inakwenda kwa pande zote kuna vitu ambavyo ukimwambia mtu ni vidogo sana ila ukificha vinakua kwa vile tu ulifanya siri.
6.Hakikisha uwezo wenu wa kuelewa unaendana.
Hapa siongelei darasa ila mnavyokua sambamba kwenye maongezi ya kawaida tu yasiyo hitaji degree.
7.Onyesha Misimamo yako hata kama unaona ni migumu kueleweka.
Ni vizuri mtu akikubali/taka
kujiingiza kwenye mahusiano na wewe awe akijua atakua na mtu wa aina
gani kama hupendi nguo fupi,mwanamke/mwanaume mnywaji wa pombe, mvuta
sigara n.k sio unasubiri mpaka muwe pamoja ndo muanze kuzozana.
8.Hakikisha kuna vitu Mnavyo Shabihiana.
Ni muhimu mkiwa na vitu
mnavyoweza kufanya pamoja iwe ni kuangalia movie ama kutembea nyakati za
jioni inasaidia kuimarisha ukaribu wenu kuliko kila mtu kwenda na njia
yake.
Comments
Post a Comment