USIRUHUSU SIMU YA MKONONI IWE SUMU KATIKA UHUSIANO WAKO


Miaka ya nyuma, hususan wakati simu za mkononi zilipokuwa hazijaingia nchini, matatizo kwa wanandoa au wapendanao yalikuwa machache sana kulinganisha na sasa baada ya ujio wa simu.

Ni wazi kwamba katika migogoro mingi ya mahusiano simu imekuwa kichocheo kikubwa cha wapendanao au wanandoa kugombana. Simu ndizo zinazoleta uhasama na kuvunja ndoa nyingi. Simu ndizo zinawafanya watu wengi waliopo kwenye uhusiano kugombana.black-couple-3

Bahati mbaya sana, kati ya kesi nyingi za simu, zipo ambazo zinakuwa na ukweli lakini nyingine huwa hazina ukweli. Mtu anaanzisha ugomvi kwa sababu tu ujumbe wa kimahaba umeingia kwenye simu ya mke au mumewe.

Hahitaji kuhoji. Anapoona tu ujumbe umeingia, kinachofuata ni ugomvi kwa mwenzi wake. Atamtukana, atampiga na atafanya kila linalowezekana
kuhakikisha anaondoa hasira zake kwa kile alichokiona.

Kumbe pengine angejipa nafasi ya kutafakari, akahoji, labda hata wasingefikia hatua ya kugombana. Anaanzisha ugomvi kumbe yule aliyetuma ujumbe huo, mwenzi wake wala hamjui.

NINI CHA KUFANYA?

Suala la kwanza unalopaswa kufanya kabla hujaingia kwenye uhusiano, mchunguze vizuri mhusika. Hakikisha ni mtu mwenye moyo wa kuridhika.black-couple

Ninaposema moyo wa kuridhika nina maana gani? Awe tayari ameshaamua kuwa ‘serious’ na mtu mmoja. Macho yake si ya kutangatanga. Hababaishwi na kila mwanamke au mwanaume amuonaye. Mtu wa aina hiyo hafai. Atakupotezea muda. Atakusababishia ugomvi kila wakati mbele ya safari. Anzisha uhusiano na mtu aliyetosheka na ujana.

UAMINIFU

Ukishafanikiwa kuwa na mtu mwenye sifa hizo, kinachofuata ni suala la uaminifu. Jenga imani kwa mwenzako. Mfikirie katika fikra chanya zaidi na si hasi. Muamini kwamba hawezi kukusaliti. Ukimuwazia mwenzako katika mazuri ni rahisi hata kukabiliana na wazushi watakaokuletea maneno ya uongo ili kukugombanisha na mwenzi wako.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016