Taarifa za uzushi kuhusu kifo cha muigizaji Muhogo Mchungu.
Kumeibuka taarifa zisizo sahihi
ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii haswa Whatsapp na
Instagram kuhusiana na muigizaji mkongwe wa filamu Tanzania, Muhogo
Mchungu kufariki dunia. Baada ya taarifa hizo kuenea, kupitia mtandao
wake wa Instagram, mwigizaji wa bongomovie Batuli amekanusha taarifa
hizo.
Batuli aliandika hivi…
”Muogopeni
Mungu Nyie Mnaozusha Habari Za Vifo Kwa Watu Maarufu,, Mkumbuke Hakuna
Atakayepaa Sote Njia Yetu Ni Moja, Tumieni Mitandao Vizuri Sio Sifa Wala
Ujanja Kutengeneza Habari Zenye Uzushi Kila Baada Ya Muda Fulani, Kifo
Ni Cha Wote Hakikimbiliki Mtambue Ipo Siku Na Nyie Mabingwa Wa Kuzusha
Kitawatembelea Tu #MunguAnawaona#MolaAkupeMaishaMarefuBaba”
Comments
Post a Comment