KUJAMBA NA SABABU ZAKE KISAYANSI
BINADAMU na viumbe hai kwa ujumla tunasifa ya kupumua kupitia mifumo mbalimbali ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka katika miili yetu,kupumua huku si tu kunatufanya kutimiza moja ya kazi na sifa ya mwili bali pia huwa ni kama tiba kwa upande mwingine.Kwa kawaida Binadamu hupumua katika hali ya kuvuta hewa na kuitoa nnje,kujisaidia haja kubwa na ndogo lakini kupumua kwa kutoa hewa kupitia kinywa,makalio(kujamba) na vinyweleo katika ngoziKwanini tunajamba? kwanini “ushuzi” unanuka?Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.Kila mtu anajamba,hata Oliver queen nae hujamba.
1.Kujamba ni nini hasa?Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida “ushuzi” unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.Asilimia moja tu ya “ushuzi” inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya “ushuzi” utoe harufu mbayaKujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na “vibration” katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea “presha” inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.
2.Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage,kabichi,soda na mayai.
3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku.Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.
4.Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.
5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya YakoMadaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.
Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi,na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).
Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi,na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).
Comments
Post a Comment