HEKAHEKA: Jamaa katapeli, katumia njia ya msiba, kahakikisha mpaka kaburi limechimbwa
September 7 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib amekutana
na hii iliyotokea Mburahati Dar es salaam ambapo Jamaa aliyewahi
kutapeli msikitini mwezi wa Ramadhani akidai kutaka kufuturisha.
Sasa jana
September 7 2016 kaenda tena maeneo ya Mburahati ambapo ameefanya
utapeli wa aina yake kwa kuwachimbisha watu kaburi na kuwaibia simu na
kutokomea, kama hukupata nafasi ya kuisikiliza usijali millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye Hekaheka ya leo.
Moja ya mama waliotapeliwa matofali ya kujengea kaburi anasema……>>>aliomba
simu yangu wakati vijana wanapeleka matofali akaenda, akongea kuulizia
kuhusu mpishi, akawa anauliza fundi mzuri tunampata wapi, akasema ngoja
nimwangalie kuna kijana yuko hapa nyuma akaondoka na simu sikuwa na
wasiwasi kwa sababu kuna kijana alikuja naye
>>>vijana
wangu walirudi kuchukua trip nyingine ya tofauli wakaniambia
umeshachukua hela nikasema bado wakasema chukua kwanza hela, namsubiri
hakutokea, nikachukua simu nyingine nikapiga simu yangu haipatikani,
nikamuuliza yule mwenzie akasema mimi nilikutana naye njiani akaniuliza
tofali nzuri nikaja naye
Unaambiwa katapeli mwenye bodaboda, mwenye gari lililokuwa linachukua tofali, mama muuza chai, muuza nyama na mchele.
Comments
Post a Comment