Skip to main content
MAPENZI YANAUMIZA LAKINI YANASAHAULIKA….
Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa
kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo
yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote
unachokijua chenye kusababisha maumivu.
Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa
na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila
siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika
kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine
wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia.
Inawezekana ni kweli mpenzi wako
amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na
ninaamini ipo siku utayasahau. Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke,
mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi
kinavyoikumba ardhi, mara nyingi huwa ni kwa mpito.
Kuna msemo ambao hutumika sana katika dunia tuliyonayo usemao “hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”.
Hakika maneno haya yana ukweli fulani ndani yake na ndivyo ilivyo
kwamba, mapenzi yanaumiza, yanatesa, yanasumbua ila maumivu yake yana
mwisho. Haijalishi umeumia, umeteswa kwa muda au namna gani lakini amini
siku yaja nawe utapona na kurudi katika hali yako ya zamani.
Usimchukie aliyekuumiza na kukutesa
katika mapenzi, amini ni sehemu ya maisha yako, ulipaswa kuyapita.
Wapenzi wengi wamekuwa wakiteseka mno na namna ya kuwasahau wenza wao
baada ya kutengena au kuachwa.
Comments
Post a Comment