HIVI UNAITAMBUA THAMANI YA ULIYENAYE ?


Najua wote tunajua thamani ya mapenzi na pia tunafahamu ni jinsi gani mapenzi yanatesa, yanaumiza na wakati mwingine kuua. Wengi tunafahamu jinsi mapenzi yalivyoleta umoja, undugu na urafiki ambao haukutarajiwa katika maisha yetu lakini kutokana na huyu kuoa yule na yule kuolewa na huyu tumejikuta tukiunganishwa na jambo hilo.

Licha ya kujua thamani ya mapenzi na maumivu yake lakini tumeshindwa kuilinda thamani na kuyapuuza maamuvi yake. Tumekuwa wakosaji wakubwa sana kwa wenza wetu tulionao. Tumekuwa hatutambui thamani ya tulionao mpaka pale wanapoondoka mikononi mwetu. Tumekuwa watu tusiothamini mioyo na machozi ya wenza wetu kanakwamba sisi ni wanyama.

BLACK MANKwanini umlize mwanaume aliyekupenda na kukusaidia katika maisha yako? Kwanini umsaliti mwanamke aliyekupa mwili wake na moyo wake pamoja na kukupa thamani kubwa katika maisha yake? Ipi thamani ya machozi yake kwako? Ipi thamani ya mapenzi yake kwako? Kwanini uliache penzi lako lenye furaha na kwenda kwa mtu mwingine ambaye wakati mwingine anaweza asifike hata nusu ya uliyenae?

Kumbukeni mapenzi ni hisia ambayo hukaa ndani kabisa ya moyo, hisia ambazo haziwezi kupuuzwa au kutokuthaminiwa. Hisia ambazo zinauwezo wa kukubadili jina kutoka fulani na kuwa marehemu fulani. Hisia ambazo huumiza zaidi ya kufiwa na ndugu na wakati mwingine hata wazazi wako. Mwanamke au mwanaume anapokupenda huwa amekuona wewe na kukuchagua wewe kati ya wengi ambao amewaona.BLACK WOMAN

Amekuchagua wewe kwa kuamini kuwa wewe ni faraja, furaha, liwazo na kumbatio la huba. Hakukupenda ili umsaliti na kuishusha thamani yake. Hakukupenda ili umpange foleni na kumvunjia heshima, bali amekuoa kwa kuamini wewe ndio kila kitu katika maisha yake. Kama ni hivyo kwanini usimtunzie heshima yake? Kwanini usiipiganie thamani yake? Mwanamke aliyekupenda kweli unaweza ukamuacha akalia? Mwanaume uliyempenda kweli unaweza kumuacha akilia? Ni ipi thamani ya upendo wenu? Ni ipi heshima ya mapenzi yenu?.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016