Familia ya Diamond Yaikacha Sherehe ya Birthday ya Zari Iliyofanyika Zanzibar...Mabifu Yaibuka Upya

MWISHONI mwa wiki iliyopita (juzi Ijumaa usiku) ilifanyika pati ya kusherehekea kuzaliwa kwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ambayo imeibua mabifu upya. Pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa wachache kutoka Bongo ambao ni pamoja na Moze Iyobo, Aunt Ezekiel na wengineo ilifanyika Zanzibar ambapo licha ya kufana, imeibua mtifuano upya kati ya Zari na wifi yake, Esma Abdulkadiri na Diamond na mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga.

IVAN NA DIAMOND
Bifu la wawili hawa lilikuwa limezimika, lakini lilirudi upya baada ya juzikati Diamond kumzawadia Zari nyumba iliyopo Afrika Kusini kisha kumrushia Ivan dongo kwa kuandika mtandaoni: “Wanakazana kujisifu matajiri ilhali watoto wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga… halafu leo yuleyule wanayemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa maskini, kajawa na shida, kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa.”

NI DONGO KWA IVAN
Ujumbe huo moja kwa moja u l i o n e k a n a kumhusu Ivan ambaye kipindi cha nyuma kwa kushirikiana na mshikaji wake aliyefahamika kwa jina la King Laurence, walikuwa wakimtusi wakimsema kuwa ni maskini ila wao wana pesa licha ya madai kuwa, nyumba wanayoishi watoto wa Zari kule Sauzi ni ya kupanga. Baada ya dongo hilo, hali ilichafuka huku Ivan akimrushia madongo Diamond sambamba kumtaka Zari amwambie bwana wake (Diamond) aondoe ujumbe huo mtandaoni kwani hata wanaye wakiuona wataumia. Inadaiwa kuwa, licha ya Ivan kuomba hivyo, Zari alimjibu kuwa Diamond amegoma kwa maelezo kwamba, wao (King Laurence na Ivan) ndiyo walioanza kumtusi.

 ESMA NA ZARI
Bifu lao lilihusishwa baada ya Esma kuulizwa sababu za kutomuwish wifi yake katika siku yake ya kuzaliwa, kuonesha ‘analo na limemfika hapa’ alifunguka: “Siwezi kumuwishi, mbona Taraj (mwanaye) hakumuwishi wakati ndiye aliyekuwa akicheza na mwanaye (Tiffah) nyumbani? Wee ukosane na mimi umkasirikie hadi mtoto, ujinga huo. Siwezi kumuwishi Mbona Bi. Snura (mama wa Diamond) alimuwishi akamfuta na mafumbo juu, akasababisha watu wakamchamba!….. (anataja jina la mwandishi) nimekaa tumboni kwa mama yangu miezi 9 ‘so’ mtu anavyomletea dharau siwezi kumpenda. Mbona wote tumekaa nao vizuri haijawahi tokea haya mambo, kwa nini yeye?” alihoji Esma.

FAMILIA YA DIAMOND YASUSA BETHIDEI
Katika kile kinachoonesha kuna kitu kizito nyuma ya pazia kati ya Zari na ndugu wa Diamond, inadaiwa hakuna hata mmoja aliyefika hali iliyoibua maswali mengi.

DIAMOND, ZARI VIPI?
Kufuatia kuibuka kwa mabifu hayo sambamba na figisu nyingine, gazeti hili lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Zari kupitia simu zao za mkononi ili waseme lolote, lakini simu zao hazikuweza kupatikana.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016