MBINU ZA KUMTOKEA USIYEMJUA SIKU YA KWANZA



Unataka kuzungumza na mwanamke ambaye humfahamu? Kuongea na mwanamke ambaye humjui ni kama vile kujaribu kuoga na maji baridi. Inakuwa vigumu na inakufanya kuingiwa na kibaridi. Kila wakati unapochukua hatua ya mbele unasikia kama tumbo linakukoroga vile.black-6

Lakini kama mwanamume, jinsi ya kutongoza mwanamke ni jambo muhimu la kujua likija suala la mapenzi. Kile ambacho kinachohitaji kwanza kabisa ni kumfanya mwanamke kama huyo akutambue yaani upate kufahamika kwake. Hii inakuwa rahisi kwa kutumia mbinu hizi;

Mwangalie

Tuseme saa hizi uko na marafiki zako ama uko peke yako katika sehemu ambayo ina watu wengi halafu huyo mwanamke unataka kumtongoza  yupo karibu na wewe ama sehemu mbali kidogo na wewe.black-3

Kile unachohitajika sasa ni umuangalie ili ufanye kumuonesha kama unajaribu kumuangalia yeye. Jaribu kujifanya unamuangalia kisirisiri, halafu akijaribu kukuangalia tu unajifanya unashughuli nyingine ama unaongea na marafiki zako. Hii itamsisimua kutaka kujua kwanini unamuangalia hivyo itamfanya na yeye kukuangalia mara kwa mara kama utakuwa ukimwangalia.

Mwangalie machoni

Kila wakati akikuangalia, wewe muangalie halafu papo hapo uangalie kando kikondoo. Endelea kumuangalia kimtindo huo mara kwa mara na wakati mwingine, mwangalie nusu sekunde, uangalie kando halafu hapo hapo muangalie tena, ukifanya hivyo utakuwa unamsisimua kihisia. Lakini kama umejaribu njia hii yote halafu hakuonesha dalili ya kuingiliana basi itakuwa hajakupenda ama kuridhika na wewe.black-1

Jifanye kutoeleweka

Kama uko na marafiki zako, muangalie mara kwa mara, lakini jifanye kama unasumbuliwa na jambo fulani ambalo linakufanya wewe usielewe kile ambacho marafiki zako wanaongea. Hii itamfanya yule mwanamke kufikiria kuwa ameingia kwa akili yako hivyo ataona ya kuwa yeye ndiye chanzo kikuu kinachokuzuia wewe kumakinika na yale ambayo marafiki zako wanaongea.black-4

Mwonyeshe tabasamu

Bila kupoteza wakati, hii itakuwa ufunguo wa kwako kufungua mlango wako wa kuongea naye kwani akili yake yote  itakuwa imekuja kwako hivyo lile unalohitajika la kufanya ni kumwonyesha tabasamu. Fanya kutabasamu  kiasi tu ili kuonyesha kuwa wewe umevutiwa nae.black-5

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016