Jinsi ya Kumlinda Mumeo Asichepuke

Wanawake wengi hawajui nafasi ya mume, hivyo kufanya mambo kiholela na kujikuta NDOA inaanza kuleta matatzo.

Jinsi ya kumlinda mumeo:

1. MAPISHI
Unapokua upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa anaekula ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri. Wanawake wanapika chakula kizuri siku za sikukuu ndo anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani.
Au siku ukisikia mumeo anakuja na mgeni rafki yake alafu yamkini ni mtu mwenye cheo fulani ndo unataka upike vizuri.
KWA IYO USITAKE KUPIKA VIZURI ETI KWA SABABU KUNA MGENI AMEKUTEMBELEA BALI IWE NDO TABIA YAKO KWA MUMEO

2. USAFI
Wanawake bado hawajajua kuwa usafi ni kivutio pia kikubwa kwa mwanamume. Na kama tunavyojua kuwa usafi maana yake ni "kila kitu mahali pake"
Sasa wanawake utakuta vijiko vya chakula vipo kwenye kitanda eti kwa sababu tu ana mtoto mdogo. Au nguo za mikojo ya mtoto unaweka chini ya kitanda mpaka zinaanza kutoa harufu. USAFI NI MUHIMU SANA, IWE KWAKO MKE, AU MAZINGIRA YA NYUMBA. NA HAPA SIMAANISHI KUWA MSAFI KWA MAANA YA KUJIPODOA.

3. MANENO MAZURI
Mke ni lazma ujue maneno ya kuongea na mumeo. Maneno mazuri yatamlinda mumeo pale atakapoyasikia kwa wengine. NA HATA KAMA MUMEO HATAONYESHA KUJALI, BADO WEWE MKE UNATAKIWA KUENDELEA KUKAA KWNYE HIYO NAFASI.

Mungu akusaidie ewe mke kuitumia nafasi yako.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016