AJALI TABATA MATUMBI DSM, WENGI KUPOTEZA MAISHA
Ajali mbaya imetokea leo matumbi jijini Dar Es Salaam ikihusisha daladala(DCM) la G/Mboto-Ubungo na Lori la Mizigo pamoja na Lori lililokuwa limebeba ng’ombe.
Daladala DCM inasemekana kuwa walionusurika si zaidi ya watu watano, na malorini, wote wamefariki dunia.
Abiria waliokuwemo ndani ya daladala DCM walishuhudiwa kujaa sana na wengine wakiwa wamesimama hali ambayo imesababisha wengi kupoteza maisha.
Haijajulikana chanzo cha ajali ni nini mpaka sasa, @mautunduyabongo itaendelea kukupa taarifa zaidi.
Pole za dhati ziende kwa wafiwa na Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
Majeruhi, kwa jina la mola yeye alie juu, poleni na tunawaombea kupona na kuendelea na maisha. Amen.
Follow instagram @mautunduyabongo
Comments
Post a Comment