Watu Watano Wafa Kwa Kufunikwa na Kifusi Wakati Wakijaribu Kuchimba Mawe Waliyodhania ni Dhahabu
Watu watano wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwa kuvunjika viungo vyao baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu.
Tukio hilo limetokea jana saa 9:00 Alasiri, katika kata ya Mgusu Wilayani Geita ambapo watu hao waliangukiwa na ukuta wa udongo waliokuwa wakiuchimba.Wakizunguza na channel Ten iliyofika katika kata hiyo baadhi ya wachimbaji waliokutwa katika eneo hilo wakaeleza hali ilivyokuwa.
Pamoja na tukio hilo la kusikitisha wachimbaji hao wakatoa kilio chao kwa Serikali kuhusu maeneo ya kuchimba yaliyo salama ikiwa ni pamoja na kuwapa zana za kuchimbia na uokoaji.
Katibu tawala ya wilaya ya Geita Gaspar Kanyaiita aliyetembelea eneo hilo ameagiza Ofisi ya Madini kuwakamata wachimbaji wote wanaokiuka kanuni huku kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita akisema eneo hilo limefungwa tangu jana mpaka itapotangazwa utaratibu mwingine
Comments
Post a Comment