Diamond Platnumz akutana na Kanye West, Los Angeles
Diamond Platnumz amekutana na rapper ambaye watu wengi wangependa kukutana naye na kuongea mawili matatu kutokana na heshima yake, Kanye West.
Najua kuwa Diamond na Kanye wana kitu kimoja wanachofanana – wote wanapenda fashion kwahiyo kwa hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ kukutana na Yeezy hata kwa dakika chache tu ni kitu alichokipokea kwa heshima kubwa.
Bila shaka Diamond alikutana na rapper huyo aliyeachia album mpya The Life of Pablo hivi karibuni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, LAX.
“LA am in Town Baby!!!….. With my bro #WEST,” aliandika Diamond kwenye picha aliyopost Instagram.
Hata hivyo mwisho wa safari yake ni Las Vegas.
“Duh tangu jana saa 10 jioni nipo kwa mandege tu [disappointed_relieved] ….What a Long a** flight!…. Still gat 28 mints to land in LA, then wait for 4 hrs transit….then connect from LA to Las Vegas,” aliandika kwenye picha hiyo chini.
Comments
Post a Comment