Juma Jux Asema Hataki Maswali ya Vanessa na Jack...
JUX cameweka wazi hisia zake hizo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz ambapo alisema kuwa yeye pia ni mwanamuziki kama ilivyo kwa Vanessa Mdee na kusema kuwa imejengeka kuwa kila interview anayoifanya ni lazima watu wamuulize kuhusu uhusiano wake na Vanessa na kwasasa imeibuka ya kumuuliza juu ya Jack Cliff.
Jux alishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ‘video vixen’ Jack Cliff ambaye anashikiliwa nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya na kwasasa staa huyo anajihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Vanessa Mdee.
Jux anasema kuwa kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye interview ambayo yatakuza muziki wake mbali ya kuzungumza mambo ambayo yatakuwa hayasaidii mahusiano yake wala muziki wake.
Comments
Post a Comment