Ray C Akana Kurudia Madawa ya Kulevya...Apanga Kuvishitaki Vyombo vya Habari
Msanii Ray C amevijia juu vyombo vya habari vinavyoandika taarifa za uongo juu yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii atavifikisha mahakamani.
Katika ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.
“Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule wa kipindi na enzi hizo now I'm not catalysts of drugs, hata hivyo tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa nyumbu” aliandika Ray C.
Pia Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika wa madawa ya kulevya.
“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”,aliandika Ray c.
Comments
Post a Comment