Harmonize Atoboa Siri 'Ni Kweli Zari Hassan Ndio Aliniunganisha na Huddah Baada ya Kumtamani Kwa Muda Mrefu'
Siri
nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa
kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji
yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi
nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.
Akizungumza
ndani ya Makao Makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini
Dar, wikiendi iliyopita, Harmonize alisema kuwa kwenye maisha yake
hakuwahi kuwa na ndoto ya kukutana laivu na Huddah lakini bahati hiyo
aliipata akiwa nchini Afrika Kusini baada ya kukutanishwa naye na Zari.
“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa na Mautundu ya Bongo.
Comments
Post a Comment