Belle 9: Mimi Sina Tatizo na Diamond, ni Baada ya Watu Kuhack Akaunti yake na Kumtukana Diamond


Watu wasiyo julikana wamehack akaunti ya facebook ya msanii Belle 9 na kuweka post yenye picha ya msanii Diamond na kuandika maneno yanayoashiria matusi ya nguoni.Belle99Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Belle 9 amesema yeye anajulikana sio msanii wa kufanya vitu kama hivyo.“Mimi sina tatizo na msanii wala sina upande wowote,” alisema Belle 9.
“Hili ni tatizo kama matatizo mengine, ni geni kwangu kwa sababu halijawai tokea lakini kwa wasanii wengine yalishatokea. Kwa hiyo naweza sema bado watu wangu wanaendelea kurekebisha tatizo na kuirudisha akaunti yangu. Mimi naimani kuwa watu wameelewa kwa sio mimi kwa sababu mimi sio mtu wa mambo hayo,” aliongeza Belle.

______________________

Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu