Mwimbaji Vanessa Mdee Amfungukia Laivu Jack Patrick Aliyoko Jela....
V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack.
Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.
“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.
Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposika amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:
“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria.
“I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.
Comments
Post a Comment