Maoni: Hofu yangu Kuhusu Label ya Wasafi, Diamond, Harmonize na Raymond ni Kama ‘Mtu Mmoja’
Makala imeandikwa na Wynjones Kinye (Mhadhiri chuo kikuu cha SAUT)Naappreciate sana juhudi za Diamond katika kuunyanyua muziki wa Tanzania kwa kuibua vipaji vipya kama Harmonize, Raymond na watakaofuata kama wapo.Ni dhahiri kuwa kwa hili la kusimamia vijana wawili tu kiasi kikubwa cha fedha kimetumika na kinaendelea kutumika hasa ukizingatia kuwa Diamond tayari ni mtu sensitive kwenye quality ya product, na tunajua kuwa quality ni gharama kubwa siku hizi kama sio siku zote.
Diamond amethubutu kuwekeza, kibiashara tunategemea return katika kila unachofanya ‘kibiashara’ hivyo ni muhimu sana kufikiria vitu vingi vya kuifanikisha biashara ukiachana na mtaji.
Hata kama una mtaji mkubwa na fedha za ziada kuuendeleza mradi bado failure iko pale kama hutotazama vitu vingine kwa kina.Licha ya nguvu nyingi anayoweka Diamond kwenye muziki wa vijana wake ‘publicity na video nzuri’ bado mimi nina hofu ya kufanikiwa kwake kuwafikisha vijana wake hawa chini ya label yake.
Nilivumilia kulisema hili baada ya kumsikiliza Harmonize, ila sasa nimeshindwa kukaa nalo baada ya kumsikia Raymond.Naadmit kuwa hawa vijana Raymond na Harmonize wana vipaji vikubwa, wana sauti nzuri sana na ni waandishi vizuri lakini wanakosa kitu cha kuwafanya kuwa brand.
Yupo mwandishi mmoja anaitwa Angela Cross alisema…“Your brand is the foundation of your relationship with your audience – so be mindful of who your audience is (and no, it’s not “everyone”), what they want, and how you can connect with and serve them.”
Najua brand ni neno pana na kila mtu anaweza kulitetea kivyake kutokana na mapenzi na uelewa kwenye suala husika, vyovyote iwavyo niseme Diamond, Raymond, na Harmonize ni “MTU MMOJA.”
Yaani ukitoa sauti zao (ambazo pia sasa zinaelekea kufanana) vingine vyote ninafanana zaidi.Hapa nazungumzia uandishi wao, mawazo yao katika nyimbo, mtindo wa nyimbo zao, uandishi wao, na strategies za kibiashara ambazo nawez
Comments
Post a Comment