Diamond Platnumz akisema kitu kilichomfanya Kanye West kutaka kupiga naye picha.
Baada ya picha ya staa wa bongo fleva Diamond Platnumz akiwa na Hip Hop staa kutoka Marekani, Kanye West kusamba pamekuwa na maswali mengi ya Ilikuaje mpaka picha hii ikapigwa?
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema,
“Nilipokuwa airport pale Los Angeles tunasubiri kuchukua mabegi yetu, nilisikia mtu akisema ninaweza kupiga picha viatu vyako? Kwakuwa alikuwa ameinama sikuweza kumtambua lakini alipoinuka nikashangaa kumuona ni brother Kanye West. Nilimuomba tupige picha kwanza halafu vingine vitaendelea.”

Kuhusu collabo D alisema“Tumuombe Mungu mambo yaendelee vizuri kama tulivyopanga, kuna kitu kizuri kinaweza kikatokea kati yetu"
Comments
Post a Comment