Baada ya Chid Benz Kukiri Kuwa Anahitaji Msaada..Babutale Ajitosa Kumsaidia....


Picha za Chidi Benz zilizomuonesha akiwa amedhoofika afya yake ziliwashtua wengi. Yeye mwenyewe alikiri kuwa anahitaji kusaidiwa.Na sasa huenda msaada anaouhitaji umemfikia.
Babutale amepost video Instagram akiwa na rapper huyo na anasikika akisema: Mungu tusimamie huku Chidi akisema: Mungu tusimamie, tusaidie, mjalie Tale nijaalie na mimi, tunaomba mengi tutakuwa na vingi, tutaenda sehemu nyingi tutafanikiwa.
Tale alimalizia kwa kusema ‘inawezekana, Chidi kaamua.’Haijulikani hasa ni nini kimepangwa kufanyika lakini la msingi ni kuwa umoja wa wasanii umeonekana kutomwacha Chidi apotee.
Hata hivyo katika hatua iliyowashangaza wengine, rapper Young D amemtupia lawama Babutale kwa kuweka video hiyo.
“Nimeona hii post nikajiuliza! Kwa hali Kama hii sio mwanzo mzuri kama ni mwanzo wa kumsaidia chidi.. Haonekani vizuri! Challenge kwako blaza hii ni aibu sidhani Kama kuna die hard fan wa ukweli wa chidi Kama ataipenda hii Au ata Kama ni kweli una mpango wa kumsaidia kama manager bora Afrika..! Nimeiona hii nmeshtuka tale! @babutale umeniangusha Kwa hili.. Starting to heal but kill the best rapper mbele ya macho ya waTZ.”

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016