Juma Nature Adai Mshindani Wake Kwenye Muziki kwa Sasa ni Diamond
Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature amedai msanii pekee ambaye anaweza akashindana naye kwa sasa ni Diamond.
nature
Akizungumza na tovuti ya Times Fm, Juma Nature ameomba wadau kuandaa tamasha ili washindanishwe.
“Watu
wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani atakamua, unajua
tuseme ukweli bongo flava sasa mimi na Diamond ndio wapinzani pekee,”
alisema Juma Nature.
Aliongeza, “Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe na mimi nguvu yangu ilivyo mtaani,”
Nature amesema anaamini muziki wake aliyokuwa anafanya zamani una nguvu kubwa kuliko huu wa wasanii wa sasa.
Comments
Post a Comment