Umaarufu wamfanya Harmonize aishi kwa shida


Msanii kutoka lebo ya WCB Harmonize, ametoa siri ya maisha ya wasanii ambao wako chini ya lebo hiyo, ambayo inawafanya kuepuka mambo mengi ikiwemo skendo chafu, huku akidai kuwa wanafuata nyayo za bosi wao Diamond Platnums.Harmonize ameongea hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kuwa wao kama WCB hawana kawaida ya kwenda club kutokana na kubanwa na majukumu, na pia hata bosi wao ambao ni mfano mzuri kwao, hana kawaida ya kwenda sehemu kama hizo.

“Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda club sitokagi, kwa sababu pale ofisini kuna studio studio mle mle ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind, kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza kupitia yeye”, alisema Harmonize.

Pia Harmonize amekiri kuwa umaarufu alionao sasa ndio unamfanya ashindwe kwenda sehemu mbali mbali pamoja na kujichanganya na wasanii wengine, kutokana na kutozoea mazingira hayo, huku akitamani maisha aliyokuwa nayo kabla, lakini pia kuna muepusha na skendo mbaya.

“Juzi kulikuwa na mwaliko Mh Rais alialika wasanii Ikulu, mi sikuenda kwa sababu sijazoea hayo mazingira, kwa hiyo inakuwa ngumu kuhusishwa na skendo huyo mwanamke nakutana nae wapi, sababu muda wa kutoka nakuwa sina, mi sikutanagi na wasanii wenzangu yani, muda naukosa kabisa, na ndo kati ya vitu ambavyo navimisi kabisa”, alisema Harmonize

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016