Akina Dada Msipende Kuwadharau Vijana Mnaofanya nao Kazi Maofisini...
Akina dada nipende kuwashauri kitu kimoja.
Msipende
kuwadharau vijana mnaofanyanao kazi ofisi moja na kuwaona wa thamani
kubwa watu msiowajua hasa wa kwenye mitandao mkidhani kuwa hao ndio wana
maisha bora.
Ukweli
ni kwamba akina dada wengi wanatabia ya kuwadharau vijana wanaoishinao
wakiamini kwamba watawapata watu wenye sifa wanazozihitaji toka kwenye
mitandao ya kijamii.
Matokeo
yake kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wasiokuwa na baba au
kwa jina maarufu kama watoto wa love connect, wakishazalishwa huko
walikokimbilia na kuachwa ndio wanawaona wa thamani kubwa hawa
waliowaacha mtaani.
Ushauri
kwa wadada acheni tamaa rizikeni na vijana mnao ishi nao kwenye
mazingira yenu kwani wengi wao ni watu wenye nia nzuri kwenu.
Comments
Post a Comment