Harmonize: Nilimuuliza Diamond ni Mwanamke Gani Ameachana nae Lakini Anashindwa Kumsahau
Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema wazo la wimbo wake mpya ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond, lilikuja baada ya kumuuliza Diamond ni mwanamke ganiambaye ameachana nae lakini bado anashindwa kumsahau.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Harmonize amesema baada ya kupata wazo kutoka kwa Diamond ndipo akaanza kuandika wimbo.
“Idea ilikuja kuna siku tulikuwa kwenye gari nikamuuliza (Diamond) kuna mwanamke gari ulimpenda sana hadi leo unashindwa kumsahau, akaniambia hakuna masihara kwenye mahusiano, mimi ndio nikapata idea,” alisema Harmonize.
Aliongeza, “Nikaona kama ni Diamond sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo hayo kwenye mahusiano, hata mimi mwenyewe yameshanikuta.
Kwa hiyo nikaanza kuandika,nilivyoandika mistari yangu, nikampa producer akanipa beat nikachagua.
Baada ya hapo kwa sababu Diamond alikuwa Nigeria alivyorudi siku nipo nae kwenye gari nikaiplay akaikubali akasema na mimi nitaingiza verse ya pili,”
Comments
Post a Comment