Baba Levo: Wanaosema Shilole Kachuja ni Kina Nani?
Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Kata ya Mwanga Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa wanaosema Shilole amechuja ni kina nani hao? Baba Levo alijiuliza hilo na kuzua utata kwani baadhi ya watu walianza kuhisi kwamba watu hao ni wapenzi kutokana na ukaribu wao pindi Baba Levo anapokuwa Dar es Salaam.
Kufuatia kuzua utata kipindi cha eNEWS cha EATV kilimtafuta Baba Levo ili kutatua utata juu ya suala hilo na kutaka kufahamu kama kweli Baba Levo anatoka na Shilole, lakini Baba Levo alikana kutoka kimapenzi na Shilole na kudai kwamba Shilole anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake lakini sio yeye, na kudai wao ni marafiki tu wa karibu.
“Shilole hawezi kuwa na mtu kama mimi, unajua mimi ni kiongozi saizi hivyo huyo Shishi anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake sio mimi nikija Dar es Salaam nakaa kwangu, na kuhusu mimi kuchukua gari la Shilole na kuweka bond hizo ni stori tu kwani natambua kuna watu ambao wanataka kunichafua, lakini hawajui mimi ni mchafu kwani nilishachafuliwa sana kwenye siasa lakini wale walionichafua walishindwa wao na mimi nikashinda na kuwa Mh. Diwani.” Alisema Baba Levo
Comments
Post a Comment