JE WAJUA MAMBO MAKUU 4 MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA? KAMA HAUZIJUI BASI HIZI HAPA NIMEKUFAFANULIA KWA UNDANI ZAIDI.


Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo
mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku
moja tumepumzika kuizungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na
kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya
makosa.
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa
nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya
mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.

1.KUOGA PAMOJA.
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na
majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu.
Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.
Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao,
wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza
wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo
yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji
pandeni kitandani mkiwa wapesi.

2.KUSIFIANA.
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako. Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza. Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana
kunanogesha mambo.

3.KUELEKEZANA.
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao
wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani
yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika

4.ZUNGUMZIENI MAISHA.
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la
ndoa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016