Shamsa: Mkongo wa Wolper,Wema Amenitongoza


STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati alimwaga ‘ubuyu’ hadharani kwa kusema kwamba, yule jamaa Mkongo ambaye amekuwa akidaiwa kutoka na Wema Sepetu, Jacqueline Wolper amemtongoza.Akizungumza na kona ya Bongo Movies Shamsa alisema, hivi karibuni alienda saluni na kukutana na ujumbe wa Mkongo wa Wema, Wolper ukimuhitaji kimapenzi jambo ambalo lilimuudhi sana.“Hii si mara ya kwanza kunitongoza kwani nakumbuka kuna siku mtu aliniomba namba ya simu na baadaye nikapigiwa na huyo Mkongo akinihitaji hotelini kuongea mambo ya filamu nikamwambia amtafute meneja wangu akakataa na kung’ang’ania niende mimi nikakataa,” alisema Shamsa

Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu