Je Lulu Michael na Mama Kanumba Wanaugomvi? Lulu Adai 'Ningemkuta Mama Kanumba Uwanja wa Ndege Nisingemfukuza'


Msanii wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael alimaarufu kama 'Lulu' amefunguka na kusema kuwa yeye hafahamu sababu zilizofanya mama mzazi wa Kanumba asitokee kwenye mapokezi yake baada ya kushinda tuzo nchini Nigeria.Mtangazaji wa kipindi cha eNEWS alihoji ni sababu zipi zimepelekea Mama Kanumba kushindwa kutokea kwenye mapokezi yake ili hali Mama huyo alishiriki kwenye movie hiyo ambayo imempa ushindi Lulu Michael, ndipo hapo Lulu alipodai yeye hatambui sababu na kusema yeye alikuwa Nigeria na watu wote Tanzania walipata taarifa kupitia vyombo vya habari na ndio maana waliweza fika uwanja wa ndege kumpokea hivyo alidai hata kama angemkuta Mama Kanumba hapo ( Uwanja wa ndege) asingeweza kumfukuza.

Kauli hii ya Lulu Michael ni wazi inaonyesha huenda labda hawako sawa na mama mzazi wa Kanumba.Katika hatua nyingine Baba Mzazi wa msanii huyo alifunguka ya moyoni na kusema kwamba yeye toka awali hakupenda mwanae ajihusishe na masuala ya filamu yeye alitaka mwanae asome shule, lakini anadai kutokana na mafanikio ambayo mwanae ameyapata anaamini kuwa kweli alikuwa amepangiwa kufanikiwa kupitia filamu

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016