Idris Sultan Afunguka: Tulifanya Kosa Kubwa Sana Kutangaza Mapema Mimba ya Wema Sepetu
Maisha ya mastaa duniani hufuatiliwa kwa karibu sana na watu wengi.
Kuna kipindi yanakuwa ni asali lakini yanapobadilika huwa ni shubiri.Mwanzo mahusiano ya Idris Sultani na Madam Wema Sepetu, yalionekana kuvunjika lakini wenyewe wameonyesha kuwa bado wapo pamoja lakini wameamua kuyaficha kwa sasa.Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachoruka kupitia EATV, Idris alisema walifanya haraka kutangaza mimba ya Wema.
“Mwanzo tulifanya sana makosa kutangaza mimba ya Wema, culture yetu hairuhusu. Tulitakiwa kuweka wazi kama ingekuwa mimba imefikia miezi minne hivi na kuendelea,” alikiri.
Comments
Post a Comment