Chid Benz alimfanyia unyama Ali Kiba wakati wakirekodi wimbo ‘Hasira za Nini’
Rapper Chid Benz amesema wakati wanarekodi wimbo ‘Hasira za Nini’ aliyomshirikisha Ali Kiba, alimfungia ndani msanii huyo katika chumba cha kuingizia sauti ambacho kilikuwa na joto kali.
Ali Kiba na Chiz BenzAkizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Chid Benz alisema wakati wapo Mj Records wakirekodi kazi hiyo, Ali Kiba alidondosha chozi sababu yeye alimfungia mlango ndani na kumwambia hawezi kutoka mpaka atakapo maliza kuweka vocal.
“Unajua mdogo wangu Ali Kiba alipoingia booth mimi nikamfungia mlango kabisa ili asitoke so akawa analalamika maana mle ndani kulikuwa na joto sana, lakini nikamwambia mdogo wangu huwezi kutoka mpaka umalize kazi baada ya hapo akalia kisha akakaa zake chini baadae aliinuka na kuendelea na kazi mpaka mzigo ulipoisha ndio nikamfungulia mlango na kutoka,” alisema Chid BenzKatika hatua nyingine Chid Benz amesema licha ya yeye kufanya muziki wa Hip hop, lakini alikuwa na mashabiki wengi wakike kutokana na sauti yake pamoja aina ya nyimbo alizokuwa akiimba.
“Unajua kwangu mimi niliweza kuwa na mashabiki wa kike wengi kutokan na ukweli kwamba wanawake wanapenda sana sauti nzuri na nzito na mimi Mungu amenijalia sauti lakini pia nilikuwa naimba sana mapenzi lakini napochana kwenye mapenzi nilikuwa sifanyi zile ngumu lakini kingine nilikuwa naweza kuyaelezea vizuri mapenzi,” alisema Chid Benz
Comments
Post a Comment