Mrembo Tunda Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Tetesi Kuwa Wameachana na Yound D


Mrembo ambaye amewahi kung’arisha vichupa kadhaa vya mastaa Bongo maarufu kama Tunda amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na rapa kijana maarufu kama Young D au Paka Rapper.

Hivi karibuni kuna uvumi ulizuka kuwa wawili hao wameacha baada ya mrembo huyo kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga na Young Dee huku kati ya zaidi ya picha 480 zilizopo kwenye ukurasa wake wa Instagram amebakiza picha moja tu ya rapa huyo.

Vilevile katika ukurasa wa Young Dee kati ya picha 125 alizowahi kupiga na mrembo huyo wa vichupa ameiacha picha moja tu, jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa wapenzi wa burudani wanao wafuatilia mastaa hao.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio mrembo huyo wa vichupa amefungukia suala hilo na kueleza  kuwa yeye na Young Dee wapo sawa ingawa kuna baadhi ya maneno yake yaliashiria kuwepo jambo analolificha.

Alipoulizwa kama yeye na Young Dee ni wapenzi alijibu.”ndiyo Mimi na Young Dee tulikuwa wapenzi”, huku kitendo hicho cha mastaa hao kufuta picha limekuwa ni jambo ambalo linawatokea mastaa wengi pindi kunapotokea tofauti kati yao

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016