Tetesi ya Kwamba Ray C Amerudi Kwenye Matumizi ya Madawa ya Kulevya Isipuuzwe


Matumizi ya Madawa ya kulevya hapa nchini yanaongezeka kwa kasi sana. Huku ikionekana wasanii ni moja kati ya waathirika wa kubwa wa janga hili. Tumeona hivi karibuni rapa mkongwe Chidi Benz jinsi alivyothorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevya.Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi kwamba Ray C amerudi katika matumizi ya madawa ya kulevya ingawa mara kadhaa amekuwa akikanusha taarifa hizo.Waswahili wana msemo mashuhuri usemao ‘Lisemwalo lipo’ kwa nini asitajwe msanii wengine, na mara nyingi wasanii wote ambao hutumia Madawa ya kulevya, uanza kwa kukataa hadi pale akapozidiwa ndipo anaweka wazi.
Tumeshuhudia kwa Chidi Benz, Ray C, Q Chief na wengine.Februari mwaka huu, Ray C alikanusha vikali taarifa ya kwamba amerudi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya , “Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani it’s not easy but am a fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu, napambana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu,” aliandika Ray C katika instagram yake.

Lakini kauli hiyo bado haiendani na maisha yake halisi ya sasa, kwani Ray C bado anadaiwa kuoneka katika mitaa ya Mwananyala akiwa katika hali mbaya licha ya kuwa huu ni mwaka (3) akitumia dosi ya Methadone.Rais mstaafu Jakaya Kikwete tayari alishafanya kazi kubwa ya kumsaidia Ray C na kumfikisha hapa alipo sasa. Huu ni wakati wa wasanii wenzake kupokea kijiti na kumsaidia, Vita ya kupambana na Madawa ya kulevya ni ya wote, kila mmoja amwongoze aliyepotea njia na sio kuiachia serikali.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016