Msanii Ney wa Mitego amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa na wala hafikirii kuoa, licha ya kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi ya mama.Ney ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, na suala la kuoa kwake ni suala zito, hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa."Kusema kweli kabisa nimeulizwa swali ambalo sijaulizwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga, kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo katikati, namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia watoto, for this time nikisema nizungumzie kuhusu ndoa nitadanganya, mi sifikirrii kabisa kuhusu kuoa for this time, kwa bahati mbaya au mzuri mi sipo kwenye mahusiano, sitaki kukurupuka, unajua ukifunga ndoa kwa sisi, mi ni mkristo hiyo ndo nitolee, yani hapo ndo umejicomit umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kuzipangua tena, sifikirii kuoa, siwazi na sidhani kama nina huo mpango", alisema Ney wa Mitego.Pamoja na hayo Ney wa Mitego amekiri kuwa na mahusi...