Ukata Wamkumba Ray C, Adai Analazimika Avae ‘Ninja’ ili Aweze Kutumia Usafiri wa Daladala....Aomba Msaada Kwa Wenye Uwezo



Msanii wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema hali yake ya uchumi imekuwa mbaya zaidi hadi anashindwa kumudu baadhi ya gharama za maisha yake.

Muimbaji huyo ambaye yupo kwenye tiba ya methadone katika hospitali ya Mwananyamala kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television Jumatatu hii kuwa, anatamani sana kurudi kwenye muziki ili apate kipato chake lakini anashindwa.

“Jamani kiukweli haya maisha ya wasanii nyie acheni tu, yaani inabidi tumuombe tu mungu, mtu akikuona msanii kwenye daladala nani atanunua albamu yako, nani atakuja kwenye show yako, lakini mama ananiambia vaa ninja mwanangu nenda kapate tiba. Kwa sababu kila siku kukodi taxi ni gharama sana, kutoa elfu 25000 kutoka Bunju mpaka hospitali kila siku ni nyingi sana. Sometimes namwambia mama inabidi tutoke mapema saa 11 hivi nivae ninja twende kwanza kanisani then naweza nikachukua hata bajaji kwenda hospitali. Haya ni maisha sio kitu cha kucheka ni lazima nifanye hivyo ili niweze kumaliza dozi,” alisema Ray C.

Pia Ray C ameomba wadau mwenye uwezo wamsaidie kupush muziki wake ili aweze kujisaidia mwenyewe.

“Hakuna masharti yoyote kwenye kunisaidia, mpaka mtu akitaka kuchangia, sijui elfu 10000, 2000, jamani unaweza kunisaidia kwa namna yoyote, kiukweli mimi nahitaji kurudi kwenye game na mtu ambaye alitaka kunisaidia ameniacha,” alisema Ray C.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016