Producer wa wimbo ‘Aiyola’ wa msanii wa WCB, Harmonize, Maximizer amelikuna sikio la msanii wa Nigeria, Olamide.
|
Maximizer |
Meneja wa studio ya Kazi Kwanza ambayo Maximizer anafanyia kazi, Lawize
ameiambia Bongo5 kuwa Olamide aliupenda wimbo Aiyola baada ya kuona
wasanii wengi wakubwa Nigeria wakiupost Instagram na akapenda afanye
naye kazi.
Amesema wawili hao waliwasiliana kwenye email na Olamide anatarajia
kufanya ziara Afrika Mashariki mwezi ujao atakapotumia nafasi hiyo
kufanya kazi na Maximizer.
|
Olomide |
Kabla ya kufanya kazi kwenye studio za Kazi Kwanza producer huyo alikuwa
akifanya kazi kwenye studio za Mazu Records ambako alitayarisha nyimbo
kibao zikiwemo Pacha Wangu ya Rich Mavoko, Nakumiss ya Timbulo, Msondo
Ngoma ya Nuh Mziwanda na zingine.
Akiwa Kazi Kwanza, pamoja na kazi zingine, producer huyo ametayarisha nyimbo zote za rapper wa kike, Chemical.
Comments
Post a Comment