Sina Mpango wa Kuoa Mtu - Ney wa Mitego Afunguka..

Msanii Ney wa Mitego amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa na wala hafikirii kuoa, licha ya kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi ya mama.Ney ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, na suala la kuoa kwake ni suala zito, hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa."Kusema kweli kabisa nimeulizwa swali ambalo sijaulizwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga, kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo katikati, namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia watoto, for this time nikisema nizungumzie kuhusu ndoa nitadanganya, mi sifikirrii kabisa kuhusu kuoa for this time, kwa bahati mbaya au mzuri mi sipo kwenye mahusiano, sitaki kukurupuka, unajua ukifunga ndoa kwa sisi, mi ni mkristo hiyo ndo nitolee, yani hapo ndo umejicomit umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kuzipangua tena, sifikirii kuoa, siwazi na sidhani kama nina huo mpango", alisema Ney wa Mitego.Pamoja na hayo Ney wa Mitego amekiri kuwa na mahusiano na Mtanzania Stella a.ka Chaga Baby ambaye anaishi Marekani, lakini umbali uliopo kati yao ndio chanzo cha wao kutokuwa pamoja."Chaga baby ye yuko mbali kiukweli kabisa, labda kitu ambacho sijawahi kuzungumza kwanza kiukweli kabisa, mi nipo huku, alafu bado ana ratiba ndefu ya kuendelea kuwa kule, mi nimwanaume sitaki kuoneka mwanaume muongo ambaye anajipa matumaini ambayo hayana kichwa wala miguu, lakini wakati ukifika kama atakuja au mi nitaenda kila kitu kitakuwa sawa, but for this time niko single", alisema Nay wa Mitego._______________________

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016