Baraka da Prince kutoa ngoma na Ali Kiba,aeleza anavyomzimia.


barakaa
Msanii wa bongo fleva Baraka da Prince ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa siwezi ameweka wazi kuwa pengine baada ya wimbo wake huo wa sasa huenda akatoa ngoma ambayo amefanya na Ali Kiba.
Baraka pia amefunguka na kusema kuwa yeye ni mshabiki mkubwa wa kazi za Ali Kiba ukiachana na ukweli kwamba yeye na Kiba ni kama mtu na mdogo wake kimuziki.
Kupitia mahojiano na redio moja Baraka alisema “mimi ni mshabiki mkubwa sana wa Kiba,napenda kazi zake..nilihasa kama nahitaji kufanya nyimbo na mtu na nikamfikiria jamaa mwenyewe awe Kiba,nilipoongea akaitikia poa akaniambia kuna utaratibu niufuate kwa kuwa yeye yupo chini ya menejimenti,nikafata utaratibu tukaingia studio tukawa tumepiga kitu” alifunga Baraka na kuongeza ngoma hiyo itatoka hivi punde.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016