Skip to main content

Kenya yaifungia video hii ya 'Same Love (Remix)' inayo hamasisha mapenzi ya jinsia moja


Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya (KFCB) imepiga marufuku video moja ya muziki inayotetea haki za wapenzi wa jinsia moja. Bodi hiyo inasema kuwa video ya ''wimbo huo inakiuka maadili ya jamii''
Wimbo huo wa "Same Love (Remix)" ni chapa ya wimbo wa awali ulioimbwa na Macklemore na Ryan Lewis mwaka wa 2012. "Same Love'' unatambulishwa kama wimbo unaotetea maslahi ya wapenzi wa jinsia moja katika anuani yake ya mtandao wa video wa Youtube.
Katika video hiyo iliyochapishwa yapata juma moja lililopita na kutazamwa na takriban mara elfiu arobaini katika mtandao wa Youtube. Haijulikani kwa njia gani bodi hiyo itatekeleza marufuku yake. Mkurugenzi wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alitangaza marufuku hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.
https://youtu.be/8EataOQvPII

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 4 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016